Here's your chance to show off your #GIS skills! Send us your images by May 31 http://arcg.is/1res1pj #EsriUC #Maps
Thursday, 5 May 2016
Wednesday, 4 May 2016
MAHAFALI YA 34 YA CHUO CHA ARDHI MOROGORO
Siku ya Ijumaa tarehe 22/4/2016 yalifanyika mahafali ya 34 ya Chuo cha
Ardhi Morogoro (ARIMO), ambapo wahitimu wa Astashahada ya Awali, Astashahada na
Stashahada ya sayansi ya Geomatikia walitunukiwa vyeti. Mgeni wa Heshima
katika shughuli hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mheshimiwa Angelina S. L. Mabula ambaye aliongozana na
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bwana Yusto Lyamuya. Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Mpanduji sambamba na Kaimu Mkuu wa
Chuo cha Ardhi Morogoro Bwana Desderius Kimbe walisisimua sherehe hizo
kwa hotuba zao nzuri.
Mheshimiwa Angelina Mabula akiwa na wahitimu wa Chuo cha Ardhi Morogoro |
Wanachuo wakisoma risala |
Maandamano kuelekea sehemu yalikofanyika mahafali |
Mheshimiwa Angelina Mabula |
Mwanachuo akitoa maelezo kuhusu matumizi ya DGPS |
Wahitimu katika maandamano |
Mkurugenzi wa upimaji na ramani Bw. Lyamuya akieleza jambo wakati wa maonesho ya kitaaluma |
Mheshimiwa Angelina Mabula akifanya upimaji kwa kutumia darubini |
Mheshimiwa Angelina Mabula katika maonesho ya kitaaluma |
Mheshimiwa Angelina Mabula akiwa ofisini baada ya kuwasili katika chuo cha Ardhi Morogoro |
Mheshimiwa Angelina Mabula alipowasili katika chuo cha Ardhi Morogoro; aliye mbele yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Mpanduji. |
Mkufunzi wa chuo cha Ardhi Morogoro akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Angelina Mabula katika maonesho ya kitaaluma |
Subscribe to:
Posts (Atom)