Wednesday, 4 May 2016

MAHAFALI YA 34 YA CHUO CHA ARDHI MOROGORO

Siku ya Ijumaa tarehe 22/4/2016 yalifanyika mahafali ya 34 ya Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO), ambapo wahitimu wa Astashahada ya Awali, Astashahada na Stashahada ya sayansi ya Geomatikia walitunukiwa vyeti. Mgeni wa Heshima katika shughuli hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina S. L. Mabula ambaye aliongozana na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bwana Yusto Lyamuya. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Mpanduji sambamba na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro Bwana Desderius Kimbe walisisimua sherehe hizo kwa hotuba zao nzuri.

Mheshimiwa Angelina Mabula akiwa na wahitimu wa Chuo cha Ardhi Morogoro

Wanachuo wakisoma risala


Maandamano kuelekea sehemu yalikofanyika mahafali

Mheshimiwa Angelina Mabula

Mwanachuo akitoa maelezo kuhusu matumizi ya DGPS

Wahitimu katika maandamano

Mkurugenzi wa upimaji na ramani Bw. Lyamuya akieleza jambo wakati wa maonesho ya kitaaluma

Mheshimiwa Angelina Mabula akifanya upimaji kwa kutumia darubini

Mheshimiwa Angelina Mabula katika maonesho ya kitaaluma

Mheshimiwa Angelina Mabula akiwa ofisini baada ya kuwasili katika chuo cha Ardhi Morogoro
Mheshimiwa Angelina Mabula alipowasili katika chuo cha Ardhi Morogoro; aliye mbele yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Mpanduji.

Mkufunzi wa chuo cha Ardhi Morogoro akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Angelina Mabula katika maonesho ya kitaaluma