Walimu kutoka vyuo vitano vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hivi karibu walikuwa katika chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) kujifunza matumizi ya vifaa vya upimaji. Mafunzo hayo ya wiki mbili yalihudhuriwa na walimu kumi (i.e walimu wawili wawili) kutoka vyuo vya VETA vya Mpanda, Singida, Shinyanga, Tabora na Ulyankulu.
Picha ya pamoja wakati wa kufunga mafunzo. Waliosimama kutoka kushoto ni: Colma Charles (Mkufunzi ARIMO), Leonidas Katabalo (Tabora RVTSC), Benitho Kigava(Mpanda RVTSC), Amani Msigomba (Singida RVTSC), Niyongabo Jotham (Ulyankulu RVTSC), Said A. Kafilameno (Singida RVTSC), Mussa Mashimba (Ulyankulu RVTSC), Salu Mashimo(Shinyanga RVTSC), Tumaini Mzuma (Tabora RVTSC) na Florence Kihundo (Shinyanga RVTSC). Waliokaa kutoka kushoto ni : Cuthbert Kayumbo (Mkufunzi ARIMO), Pius Kafefa (Mkufunzi ARIMO), Eng Daudi Kadinga (Mratibu wa Mafunzo kutoka VETA) na Nkungwe Shomari (Mpanda RVTSC).
Eng Daudi Kadinda akizungumza wakati wa kufunga mafunzo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa Darasani
Unaweza kupata maelezo mafupi kuhusu mafunzo haya kwa kutazama video iliyopo katika mtando wa Youtube kwa link ifuatayo:
Siku ya Ijumaa tarehe 22/4/2016 yalifanyika mahafali ya 34 ya Chuo cha
Ardhi Morogoro (ARIMO), ambapo wahitimu wa Astashahada ya Awali, Astashahada na
Stashahada ya sayansi ya Geomatikia walitunukiwa vyeti. Mgeni wa Heshima
katika shughuli hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mheshimiwa Angelina S. L. Mabula ambaye aliongozana na
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bwana Yusto Lyamuya. Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Mpanduji sambamba na Kaimu Mkuu wa
Chuo cha Ardhi Morogoro Bwana Desderius Kimbe walisisimua sherehe hizo
kwa hotuba zao nzuri.
Mheshimiwa Angelina Mabula akiwa na wahitimu wa Chuo cha Ardhi Morogoro
Wanachuo wakisoma risala
Maandamano kuelekea sehemu yalikofanyika mahafali
Mheshimiwa Angelina Mabula
Mwanachuo akitoa maelezo kuhusu matumizi ya DGPS
Wahitimu katika maandamano
Mkurugenzi wa upimaji na ramani Bw. Lyamuya akieleza jambo wakati wa maonesho ya kitaaluma
Mheshimiwa Angelina Mabula akifanya upimaji kwa kutumia darubini
Mheshimiwa Angelina Mabula katika maonesho ya kitaaluma
Mheshimiwa Angelina Mabula akiwa ofisini baada ya kuwasili katika chuo cha Ardhi Morogoro
Mheshimiwa
Angelina Mabula alipowasili katika chuo cha Ardhi Morogoro; aliye mbele
yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Mpanduji.
Mkufunzi wa chuo cha Ardhi Morogoro akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Angelina Mabula katika maonesho ya kitaaluma